Wednesday, April 14, 2010

VIONGOZI KUDHIBITI ZANA ZA NUKLIA DUNIANI

Viongozi wa dunia waliohudhuria mkutano kuhusu usalama mjini Washington, Marekani, wamekubaliana kulinda malighafi za nyuklia kote duniani na kuhakikisha hazifiki mikononi mwa makundi ya kigaidi.

Akifunga rasmi mkutano huo, rais Barack Obama, alisema makubaliano yaliyoafikiwa ni ishara kuwa dunia sasa ni mahala salama.Viongozi hao wamesema katika miaka minne ijayo watahakikisha kuwa vitu vyote vinavyohusiana na nyuklia vinadhibitiwa.

Walitilia mkakzo umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa katika kukabiliana na silaha hizo na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa nyuklia.

Mkutano huo pia umetoa makataa ya miaka minne kwa nchi zenye zana hizo kuzidhibiti vyema na kushirikiana kuzia biashara za zana hizo.