Wednesday, April 7, 2010

MAFURIKO YAWAUWA WATU BRAZIL

Mvua kubwa iliyonyesha katika mji mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro imesababisha mafuriko yaliyowauwa mamia kadhaa ya watu.
Mitaa mingi ya mji huo imegeuka kuwa mito na maji yamesababisha matope. Mji wa Rio de Janeiro umetangazwa kuwa eneo la maafa, mvua kubwa ikiwa bado inaendelea kunyesha.
Waokoaji wameelekeza shughuli zao kwenye kitongoji cha mlima cha Shanty mjini Rio, ambako nyumba zimezikwa kwenye matope. Rais Lula Da Silva amewataka wakaazi wa maeneo hayo kuyahama makazi yao ikiwa wako katika hatari ya kukumbwa na mafuriko.

No comments: