Chama kingine maarufu cha upinzani nchini Sudan -UMMA - kimekuwa cha hivi karibuni kususia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Jumapili.
UMMA kimechukua hatua hiyo siku moja baada ya chama kikuu cha upinzani cha sudan kusini -SPLM kutangaza kuwa kitasusia uchaguzi wa Urais na ule wa ubunge katika maeneo ya kaskazini.
Mwandishi wa BBC mjini Khartoum anasema kujiondoa kwa vyama vya upinzani kunatokana na wasiwasi wa vyama hivyo kuhusu uhalali wa uchaguzi huo ambao tayari umekumbwa na shutma za udanganyifu.
Uchaguzi huu ndio wa kwanza wa vyama vingi tangu mwaka wa 1986.
Uchaguzi huu ndio wa kwanza wa vyama vingi tangu mwaka wa 1986.
No comments:
Post a Comment