Friday, April 9, 2010

LIYUMBA ATUPUNGUZIWA MASHITAKA

Amatus Liyumba


Mahakama ya Kisutu leo imemfutia shitaka kubwa la kuisababishia Serikali hasara aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba sasa hivi atabakiwa na kosa dogo la matumizi mabaya ya ofisi.


Hata hivyo Liyumba ataendelea kukaa mahabusu baada ya hakimu kukataa maombi yake ya kuachiwa kwa dhamana kutoka kwa mawakili wa utetezi, akidai kuwa dhamana ya Liyumba iliwekwa na mahakama kuu, hivyo ni mahakama hiyo yenye uwezo wa kubadilisha masharti ya dhamana.


Liyumba amerudishwa Keko. Mawakili wake wanatarajia kuwasilisha maombi ya dhamana mahakama kuu siku ya Jumatatu wiki ijayo.

No comments: