Saturday, April 10, 2010

SAA MOJA YA MAZOEZI NI MUHIMU

Huku watu wakishauriwa kufanya mazoezi nusu saa kwa siku zisizopungua tano katika wiki ili kulinda afya zao, uchunguzi mpya umesema kuwa kwa wale wanaotaka kuzuia uzito usiongezeke inawabidi wafanye mazoezi zaidi ya muda huo.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, lisaa moja la kufanya mazoezi ya wastani linatakiwa kwa ajili ya kupunguza unene kwa wanawake.

Kila ambavyo mwanamke mwenye unene wa kawaida anavyofanya mazoezi ndivyo uzito wake utakavyopungua.Uchunguzi huo umesema kuwa kushughulisha mwili kuna umuhimu mkubwa katika kupunguza unene.

Hata hivyo wataalamu wamesisitiza kwamba kufanya mazoezi kunapaswa kuambatana na kula chakula bora ili kujenga afya vyema. Pia watu wazima wameshauri kula matunda na mboga mboga, kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi na kufanya mazoezi ili kulinda afya zao na kuweza kuisha maisha marefu.

No comments: