Monday, April 12, 2010

RAIS APOKEA UJUMBE KUTOKA UVCCM MKOA WA SHINYANGA

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mchango wa jumla ya Tshs.1,482,200/- kutoka kwa jumuiya ya umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya fomu ya ugombea urais ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Makabidhiano hayo yalifanyika ikulu jijini Dar es Salaam na kushudiwa na viongozi wote wa CCM mkoa wa Shinyanga.Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Stephen Julius Masele amnaye pia alisoma ujumbe maalumu wa vijana wa mkoa wa Shinyanga.


Viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro).