Manchester United walipata pigo kubwa baada ya kuitandika Bayern Munich 3-2 lakini ushindi huo haukutosha kuwapa tiketi ya kuingia nusu fainali ya kombe la kilabu bingwa Ulaya.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita Bayern Munich waliishinda Man U 2-1.
Ingawa timu zote zilimaliza kwa mabao 4-4 Bayern Munich walitunukiwa bao la ugenini.
Bayern watakutana na Lyon ambao walifuzu kuingia nusu fainali baada ya kuishinda Bordeaux kwa jumla ya mabao 3-2. Man U walianza kwa kishindo na hata kufunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza kupitia Darron Gibson na Nani ambaye alifunga mawili.
Hata hivyo Ivica Olic aliwapa wageni bao lao la kwanza dakika chache kabla ya kipindi cha mapumziko.
Bayern waliendelea kutatiza lango la Man U mnamo kipindi cha pili hadi mchezaji wa zamani wa Chelsea, Arjen
Robben aliposukuma zinga kwenye pembe ya goli na kuzika matumaini ya wenyeji.
Manchester United ndiyo timu pekee kutoka Uingereza ambayo ilikuwa imebaki kung’ang’ania ubingwa wa kombe la Ulaya baada ya Arsenal kufungishwa virago na Barcelona hapo Jumanne. Wakati wa mechi hiyo mlinzi wa Man U Rafael Da Silva alipewa kadi nyekundu na mshambulizi Wayne Rooney akaondoka kutokana na jeraha la mguu.

No comments:
Post a Comment