Rais wa Marekani, Barack Obama, na Rais wa Urusi, Dmitry Medvedev, mjini Prague, wametia saini makubaliano ya pamoja ya kupunguza silaha za nuklia.Hii ni mara ya kwanza kwa makubaliano kama hayo kutiwa saini katika kipindi cha miaka mingi iliyopita.
Makubaliano hayo yanamaanisha kwamba pande zote zitapunguza makombora yao ya nuklia, na kila nchi kusalia na 1550.Rais Barack Obama alisema makubaliano hayo ni hatua muhimu ya kihistoria kwa upande wa suala la usalama kuhusiana na silaha za nuklia, na vile vile kwa upande wa uhusiano kati ya Marekani na Urusi.Hatua hii inamaanisha silaha hizo zitapunguzwa kwa asilimia 30.
No comments:
Post a Comment