Wednesday, April 7, 2010

SHULE YA UREMBO KUFUNGULIWA DAR

Shule maalum itakayotoa elimu na mafunzo ya kimataifa juu ya urembo, upambaji na vipodozi mbalimbali nchini inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni jijini hapa.Kwa mujibu wa mwanzilishi na mmiliki wa shule Yasmini Sharrif amesema shule hiyo itakayojulikana kama Pure Academy of Aesthetics Limited.

Yasmini alisema kuwa lengo hasa la kuanzisha shule hiyo ni pamoja na kutoa fursa kwa watanzania wanaopenda kujishughulisha na kazi za urembo na upambaji na hivyo kuwa au kuongeza ujuzi zaidi wa fani hiyo.

Aliongeza kuwa huu ni wakati muafaka wa kufungua mipaka katika elimu mbalimbali ikiwemo elimu ya urembo na vipodozi kwa kupitia shule hiyo itakayozinduliwa hivi karibuni hapa nchini.

Aidha warembo na wanamitindo kutoka sehemu mbalimbali nchini watakaojiunga na shule hiyo watapata fursa zaidi na ujuzi ambao utawasaidia hata watakapoamua kujiajiri wenyewe au hata kufundisha wenzao namna ya kutumia urembo na vipodozi hivyo mbalimbali.

Mbali na mafunzo hayo pia wanafunzi watapata fursa ya kupewa ya kupewa mafunzo na wakufunzi kutoka nje ya nchi waliobobea katika masuala mbalimbali yakiwemo ya uongozi, biashara na ujasiriamali ili kuwawezesha kujiamini pindi watakapokuwa katika biashara zao.

Mwanzilishi huyo aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawahusu hasa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 na kendelea ambapo shule itafunguliwa rasmi mwezi Julai mwaka huu.“Lengo letu ni kuwaweka katika ulimwengu wa kisasa na vilevile kuweza kufanya kazi sehemu yoyote hapa duniani.

No comments: